SERIKALI KUFIKIRIA NAMNA BORA YA KUENEZA MCHEZO WA KABADDI NCHINI
service image
25 Mar, 2023

Katibu Mkuu wa wizara ya utamaduni,Sanaa na Michezo ,Saidi Yakubu amesema Serikali itaendelea kufikiria namna bora ya kueneza mchezo huo hapa nchini .

Hayo yamesemwa Leo machi 25,2023 jijini Dar es salaam na Yakubu wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mchezo wa kabaddi duniani ambayo yamefanyika katika kituo cha utamaduni cha India (Swami Vivekandana) masaki.
Amesema kuwa wataendelea na jitihada za kuhakikisha wanaeneza mchezo huo

" Serikali kupitia BMT ndio Ilizisaidia Timu za Taifa za mchezo huo kwa gharama wakati wakienda kushiriki Afrika,hivyo Sasa zinafanya vizuri Kwa Afrika ambapo walishika nafasi ya pili zinatarajia kushiriki mashindano ya Dunia," amesema Yakubu.
Pia ameishukuru Serikali ya India kusaidia Tanzania kuleta walimu wawili Mwanamke na Mwanaume kwa ajili ya kufundisha timu za kabaddi.

 

Naye Balozi wa India Nchini Tanzania Binaya Srikanta Pradhan ,amesema wataendelea kuutangaza mchezo huo wa Kabaddi kwa kuleta makocha wa timu za taifa .

Mwenyekiti wa Chama cha Kabaddi Tanzania(TKSA ) Abdallah Nyoni, ameomba wadhamini kujitokeza kusaidia maendeleo ya michezo huo.