SERIKALI YAKAA NA TFF NA ZFF KWA MAENDELEO YA SOKA NCHINI

23 Jan, 2023
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Said Yakubu amekaa na kufanya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano baina ya pande mbili za muungano kuendeleza soka nchini.
Kikao hicho cha kimkakati kwa maendeleo ya soka nchini amekifanya leo tarehe 23 Januari, 2023 na Mashirikisho ya mpira wa miguu nchini TFF na ZFF kwa pamoja na Mabaraza ya Michezo Tanzania BMT na BMTZ katika Ukumbi wa Uwanja wa Benjamin Jijini Dar es salaam.
Aidha, Mwenyekiti wa kikao hicho Naibu Katibu Mkuu ameyataka mashirikisho hayo ya mchezo pendwa nchini kuwa na vikao vya mara kwa mara kwa afya na maendeleo ya mpira wa miguu nchini.