SERIKALI YASISITIZA UZALENDO KWA WACHEZAJI

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa akiambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi leo Juni 8, amewataka wachezaji wa Timu ya Soka ya Taifa ( Taifa Stars) kuweka uzalendo wa taifa lao kwenye mechi dhidi ya Algeria katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Ameyaongea hayo leo Juni 08, 2022 na kikosi cha Taifa Stars kabla ya kuingia uwanjani lakini pia, mchana wa leo ameyasema hayo wakati akikabidhi bendera timu ya mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu wakielekea Polland huku akiwaeleza kuwa, ndoto za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe. Samia Suluhu Hassan na watanzania ni kuona Tanzania inafanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.
"Tangulizeni uzalendo na utaifa mkiwa uwanjani huku mkitambua kuwa vipaji vyenu ndiyo mtaji wenu,"
Taifa Stars katika mechi hiyo wameambulia patupu dhidi ya Algeria waliowafunga bao 2.