GOVERNMENT GIVES INSTRUCTIONS TO PROMOTERS

Serikali imetoa maagizo kwa mapromota kuwa na ripoti ya afya kwa mabondia kabla ya kuingia makubaliano ya kusaini mikataba ya kucheza pambano.
Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 11 Januari, 2024 Dar es salaama na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma wakati wa kikao na mapromota wa ngumi za kulipwa kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na mchezo huo.
Amesema kuwa, mapromota wanatakiwa kuwa na taarifa za afya za mabondia hao kabla ya kusainia mikataba ya mapambano.
"Mapromota mnapaswa kufahamu taarifa za afya za mabondia kwa sababu mchezo huu ni hatari hivyo unatakiwa kufahamu afya zao kabla kusaini mkataba, " amesema.
Mhe. Hamis amesema kupima kwa mabondia kabla ya kusainia itamsaidia kufahamu hali ya afya zao na namna ya kujilinda kuelekea katika pambano lake.
"Jambo lingine ni bima za afya mabondia wanatakiwa kuwa nazo ili ziwarahisishie kupima afya zao kabla ya pambano na baada ya pambano ili kufahamu maendeleo ya afya," alisisitiza".