SERIKALI YAWAPONGEZA VIJANA WA MCHEZO WA JUDO BAADA YA KUONDOSHWA KWENYE MASHINDANO YA JUMUIYA YA MADOLA.

01 Aug, 2022
Serikali imewapongeza Vijana wetu Thomas Mwenda na Abdirabi Alawi Abdallah kwa kupambana vilivyo na kushangaza wengi katika mapambano yao ambayo walipoteza kwa taabu dhidi ya wapinzani wao wenye uzoefu mkubwa toka Wales na Zambia.
Baada ya kuwashuhudia vijana hao, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Saidi Yakubu @saidiyakubu1 amesema ni dhahiri kuwa wakipata mafunzo, mazoezi, vifaa na mechi za kujiandaa watafika mbali.