KIKAO NA WATAALAM WA MPIRA WA MIGUU DUNIANI

29 Jan, 2024
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha leo tarehe 29 Januari, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Bw. Grey Keenan na Hussein Skenderovic kutoka Kituo cha Dunia cha kuendeleza wachezaji wa Mpira Miguu kwa Vijana kuwa wachezaji wa viwango vya juu, Kituo hicho kipo nchini Ufaransa.
Mazungumzo hayo yamelenga kuona uwezekano wa wachezaji wa Kitanzania kupata fursa katika Kituo hicho ili kujiandaa na ushiriki wa Tanzania katika michuano ya AFCON 2027.