SPECIAL OLYMPICS KUSHIRIKI MASHINDANO YA DUNIA MWEZI JUNI 2023

07 Feb, 2023
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Y. Msitha leo tarehe 07 Februari, 2023 ofisini kwake uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, amekutana na uongozi wa Chama cha 'Special Olympic' Tanzania kwa lengo la kujadili safari ya wachezaji 20, makocha pamoja na viongozi wa michezo ya mpira wa wavu na riadha ambao wanataraji kwenda jijini Berlin nchini Ujerumani mwezi Juni mwaka huu kushiriki katika mashindano ya Dunia.