TaBSA WATAKIWA KUUSAMBAZA MCHEZO NGAZI ZOTE

Uongozi mpya wa Chama cha mchezo wa Baseball & Softball Tanzania (TaBSA) wametakiwa kusimamia na kuusambaza mchezo huo ufike maeneo mengi zaidi.
Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa uchaguzi Mkuu wa TaBSA Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Milinde Mahona, amewapongeza kwa hatua waliyofikia huku akiwataka kuhakikishe mchezo huo unaenea na kuchezwa katika mikoa mbalimbali nchini.
"Mmefanikiwa mchezo wenu unachezwa mashuleni, Ila bado haujakuwa Sana, hivyo jukumu lenu mhakikisha unaenea na kuupeleka kwa Wananchi Ili uweze kupiga hatua ya mbali,"
"Na mikoa inatakiwa kufanya mashindano yao mara kwa mara , isisubiri Chama cha Taifa,"
Ameongeza kuwa, wametangaza kuendesha ligi na kuwataka kuhakikisha klabu zote zitakazoshiriki ziwe zimesajiliwa na wanachama wa Chama kwa ujumla.
Aidha, amewataka kuandaa kanuni mbalimbali za chama na kuwasilisha kwa msajili wa vyama ndani ya miezi mitatu.
Kwa niaba ya viongozi hao wapya wa TaBSA Mwenyekiti Abdulkher Ahmed ameishukuru BMT kwa kuendelea kuwapa ushirikiano wakutosha huku akiahidi kutekeleza maelekezo kwa wakati pamoja na majukumu kwa kufuata miongozo ya serikali pamoja na katiba ya Tabsa.
Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo ni pamoja Mwenyekiti Abdulkheri Ahmed, Katibu Mkuu Alpherio Nchimbi, Katibu Mkuu Msaidizi Mwajibu Chingwaru, Mweka hazina Marcel Mutabuzi.
Wengine ni Mkurugenzi wa ufundi Softball, Mkurugenzi wa ufundi Baseball na wawakilishi wa wachezaji Antar Said na Samson Wilson.