TaBSA YAENDELEA KUJITANUA KIMATAIFA

29 Nov, 2022
Chama cha mchezo wa Baseball na Softball Tanzania kupitia mchezo wake mpya wa Baseball5 (B5) ambapo mnamo Mei, 2022 Tanzania ilikuwa mwenyeji wa mashindano ya Afrika ya kufuzu Kombe la Dunia la mchezo huo na kufanikiwa kuingia robo fainali kwa kushika nafasi ya 5 katika Afrika kwa ubora.
Hivi sasa ipo rasmi nchini Poland kwa mualiko wa Chuo Kikuu cha Olsztyn kuanzisha rasmi mchezo huu kupitia walimu wanaosomea michezo Olsztyn University.