TACA WASAJILI WACHEZAJI WAPYA

UONGOZI wa Chama Cha Chess Tanzania (TACA) umefanikiwa kuwasajili wachezaji wapya ambao watatambuliwa na Chama Cha Chess Dunia.
Hayo yamejiri mara baada ya kumalizika kwa mashindano yaliyopewa jina 'Taca Blitz chess championships ' ambayo yamefanyika kwenye kituo Cha utamaduni Ubalozi wa Urusi Dar Es Salaam.
Mjumbe wa Bodi ya TACA Albert Njau ,alisema kuwa tayari wamewasilisha majina na Sasa wanasubiria kupewa namba itakayowatambulisha na kupata fursa ya kushiriki Mashindano ya kimataifa.
Amesema mafanikio mengine ni mchezo umeendelea kukua awali ulikuwa Dar es Salaam,Sasa umeenea mikoani ukiamo Arusha.
"Mafanikio hayo yamekuwa yakiwapa moyo wa kuendelea kuwekeza nguvu ya kuhakikisha hamasa inafantika na mchezo unakuwa, na unachezwa katika mikoa mbalimbali ili kupata vipaji vingi vitakavyowakilisha kimataifa baadaye," amesema Njau.
Amesema kuwa mipango yao ni kuwa na mashindano ya Mara kwa mara ili kutoa fursa kwa washiriki kupata uzoefu wa kushiriki na kujifunza mchezo huo.
Kwa upande wa Msimamizi wa TACA Mustafa Ebrahim,alisema kuwa lengo ni kutangaza mchezo huo uweze kufika mbali zaidi, kuongeza ujuzi na viwango vya wachezaji waweze kufanya vizuri.
Ametoa wito kwa washindi na wasioshinda,na kubaini wote ni washiriki wanafursa ya kujipanga walipokosea na kufanya mazuri, wakaongeze kuboresha kwa ajili ya mashindano yajayo.
Naye mshindi wa wanawake Neema Adam, amesema kujiandaa, maandalizi na uzoefu wa kushiriki Mara kwa mara mashindano ndio Siri ya ushindi wake.
Amesema kuwa mashindano yalikuwa mazuri na ushindani, lakini Mungu amemsaidia na amefanikiwa kuibuka kuwa bingwa.
"Niwaite wanawake wenye vipaji na kuupenda mchezo huu waje kwa kwa wingi kushiriki,kushindwa ni moja ya kujifunza ,kwani hata Mimi Nina ndoto ya kuhakikisha nafanya vizuri na niwe katika timu ya Taifa ya wanawake ili nishiriki mashindano ya Olympic," amesema Neema.