TADA KUIWAKILISHA NCHI UGANDA
service image
27 Jul, 2022

Na. Najaha Bakari

Wachezaji watatu (3) wa mchezo wa vishale kupitia chama cha mchezo huo Tanzania (TADA) wataiwakilisha nchi katika mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 29 hadi 31 Julai, 2022 nchini Uganda.

Mshindano hayo yatashirikisha nchi nne (4) ikiwemo meenyeji wa mashindano hayo Uganda, Tanzania, Kenya na Sudan,

Tanzania inawakilishwa na wachezaji Munil Al Kaaf, Subira Waziri na All Miti wakiambatana na Makamu Mwenyekiti Redempta Mwebesa na Katibu Victor Kimambo ambao wameondoka leo tarehe 27 Julai, 2022.

Kwa maelezo ya Mwebesa mashindano hayo yatatumika kuchagua wachezaji bora watakaoiwakilisha Afrika katika mashindano ya dunia, huku akieleza kuwa mashindano hayo 2023 wanapendekeza yafanyike nchini Tanzania.