TADA WAISHUKURU BMT KUWAUNGA MKONO MASHINDANO YA AFRIKA MASHARIKI
service image
26 Jun, 2022


Na. Najaha Bakari - DSM

Uongozi wa Chama cha mchezo wa Vishale Tanzania (TADA) wamelishukuru Baraza la Michezo la Taifa kwa msaada waliowapa ambao umesaidia katika mashindano ya mchezo huo ya nchi za Afrika Mashariki yaliyofanyika kuanzia tarehe 24 hadi 26 Juni, 2022 katika ukumbi wa Jeshi fukwe ya Msasani Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa mashindano hayo Juni 26 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Darts Tanzania (TADA) Redempta Mwebesa, alisema kuwa wamemaliza salama na washindi wamepatikana.

"Tunashukuru tumefanikiwa na wote tulioshiriki ni washindi, hivyo wito kwa wachezaji kwenda kujipanga kwa mashindano yajayo ya wazi yatakayofanyika Septemba nchini Uganda," alisema Redempta.

Makamu huyo alisema kuwa nchi zilizoshiriki ni Kenya, Uganda, Zanzibar na wenyeji Tanzania Bara.

"Katika mashindano hayo tuligawa timu Bara ma Visiwani tukiwa na lengo la kuinua, kudumisha, kutangaza Muungano wetu na kushawishi wenzetu Zanzibar Ili waamke na kutengeneza vilabu viwe vinashiriki mchezo huu," alisema Redempta.

Timu ya taifa ya Uganda ya mchezo wa Vishale imetawazwa kuwa bingwa wa mashindano hayo yalipewa jina la Interstate ya Afrika Mashariki yaliyomalizika jana kwenye Ukumbi wa Fukwe ya Msasani, Jijini Dar Es Salaam.

Nafasi ya pili imechukuliwa na Kenya, huku wenyeji Tanzania wakimalizia nafasi ya tatu katika mashindano hayo.

Matokeo mengine ya washindi wa Mashindano ya wazi ya timu kwa wanaume nafasi ya kwanza imeenda kwa Museum kutoka Kenya, huku Tanzania ikishika nafasi ya pili na nafasi ya tatu ikimaliziwa na Kenya wakati upande wa wanawake timu ya 291DC ya Uganda imechukuwa ubingwa, nafasi ya pili KT ya imeenda kwa Tanzania.

Pia kwa wachezaji wawili wawili kwa wanaume nafasi ya kwanza na ya pili ilichukuliwa na Uganda akiwemo Kalete na Emomery na Tabaro na Katelega huku Mboyo na Antony wa Tanzania wakikamata nafasi ya tatu. Ambapo kwq upande wa wanawake Asuga na Makanga wa Uganda waliibuka washindi wa kwanza, huku Upendo na Mage wakichukua nafasi ya tatu ikienda kwa Eliza na Subira kutoka Tanzania.
@@@@@