TANZANIA KABADDI FAINALI NA MISRI
service image
26 Jul, 2022

Na. Najaha Bakari

Timu ya wanaume ya Tanzania mchezo wa kabaddi imeingia fainali kwa pointi 38 dhidi ya Mauritania ambao wameambulia pointi 4 katika mchezo wa robo fainali uliochezwa leo Julai 26, 2022 nchini Misri yanapoendelea mashindano ya Afrika ya mchezo huo.



Tanzania itacheza na timu za wenyeji Misri katika mchezo wao wa fainali kwa timu ya wanaume na wanawake.

Kwa taarifa kutoka kwa Mwenyekiti Abdallah Nyoni timu ya wanawake ilitakiwa kucheza jana na Mauritania lakini hawakuingiza timu uwanjani, Tanzania ikaingia moja kwa moja fainali ambapo ni nchi tatu tu zilizoleta timu ya wanawake ikiwemo mwenyeji Misri, Tanzania na Mauritania.