TANZANIA KABADDI WAONESHA UWEZO WAO MISRI

25 Jul, 2022
Timu ya taifa ya wanaume mchezo wa kabaddi imeaanza vizuri kwa kuwalaza Nigeria walioambulia pointi 4 dhidi ya Tanzania waliojinyakulia pointi 100 katika mechi yao ya kwanza tarehe 24 Julai, 2022 katika mashindano ya Afrika yanayoendelea nchini Misri.
Mechi ya pili Tanzania imeibuka na pointi 95 dhidi ya Kenya walioambulia pointi 5. Kesho tarehe 25 Julai Tanzania itapumzika kusubiri robo fainali kati ya timu toka kundi A mshindi wa pili ambalo ipo Egypt, Mauritania na Somalia huku kundi B ikiwemo Kenya, Nigeria na Tanzania. Hayo yameeleza na Mwenyekiti wa Chama cha mchezo huo nchini Abdallah Nyoni akiwa Misri.