TANZANIA NA SUDAN WAENDELEZA UHUSIANO KUPITIA BASEBALL
service image
15 Dec, 2022

Mashindano ya Taifa kupitia mchezo wa Baseball na Softball leo tarehe 15 Disemba, 2022 yamehitimishwa kwa kuzikutanisha timu za taifa Tanzania dhidi ya Sudan (Mchezo Maalum wa kuweka alama ya miaka 10 tokea kuasisiwa kwa mashindano haya) kwa lengo kuendelea kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo.

Aidha, mashindano hayo yalizinduliwa tarehe 11 mwezi huu kwa kushirikisha timu 10 za Baseball Wavulana na timu 6 za Softball wasichana kutoka Mikoa ya Dar Es Salaam, Pwani, Tabora, Kilimanjaro, Mbeya, Ruvuma, Dodoma na timu kutoka Zanzibar.

Akizungumzia mashindano hayo Katibu wa Chama cha Mchezo huo Alpherio Nchimbi amesema ni mafanikio makubwa sana kwa mchezo wa Baseball na Softball ndani ya miaka 10 tangu uanze wameweza kufanya mashindano ya Taifa kwa mara ya 10 bila kukosa.

Aidha, Katibu Mkuu huyo ametoa pongezi za dhati kwa Baraza la Michezo la Taifa kwa ushirikiano wanaoutoa kwao hadi kufikia hatua hiyo.

Mshindi wa kwanza katika.mashindano hayo kwa upande wa Baseball ni Azania Sekondari akifuatiwa na Zanzibar na Dodoma kushika nafasi ya tatu. Kwa upande wa Softball wasichana Bingwa ni Hondogo Sekondari ya Dar Es Salaam, mshindi wa pili ni Zanzibar na nafasi ya tatu imeenda kwa Dodoma Sekondari.