TANZANITE KUFANYIKA SEPTEMBA 2022

29 Jun, 2022
Na. Najaha Bakari - DSM
Tamasha la michezo kwa wanawake lililopewa jina la 'Tanzanite' na kufanyika kwa mara ya kwanza mwaka 2021, mwaka huu linatarajiwa kufanyika mwezi Septemba Jijini Dar es salaam.
Hayo yamebainishwa leo tarehe 29 Juni, 2022 na kamati iliyoteuliwa na Wizara yenye dhamana ya Michezo kuratibu tamasha hilo baada ya kuanza vikao vya maandalizi kuelekea tamasha hilo.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Christina Luambano Mwenyekiti wa kikao cha leo kutoka Wizara yenye dhamana ya Michezo, Halima Bushiri Katibu wa Kikao kutoka Baraza la Michezo la Taifa, Dkt. Devotha Marwa Mjumbe, Amina Karuma Mjumbe, na Rehema Jones Mjumbe, Apansia Lema Sekretarieti na Najaha Bakari Sekretarieti kutoka BMT.