TENGA AWATAKA WAJUMBE NA SEKRETARIETI KUKIMBIZANA NA MAELEKEZO YA WAZIRI

Na. Najaha Bakari
Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Leodiger Tenga amewataka wajumbe wake pamoja sekratarieti ya BMT kukimbizana katika kutekeleza maelekezo ya Waziri mwenye dhamana ya michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa aliyoyatoa wakati akizindua bodi hiyo Mei 27, 2022.
Rai hiyo ameitoa leo Julai 19, 2022 katika kikao maalum cha bodi hiyo huku akiwasisitiza wajumbe hao na sekretarieti kuwa katika suala la kubuni vyanzo vipya vya mapato aliloelekeza Waziri waangalie to nchi zingine zilizoendelea kimichezo zinavyofanya katika kuendeleza michezo.
Pamoja na kupitia utekelezaji wa maelekezo tofauti ya Waziri, Tenga amewaeleza dhamira yake kabla hajamaliza awamu ya pili BMT ni kuona michezo inachezwa shuleni kwa kufuata mitaala.