TENGA: YATUMIENI VYEMA MAFUNZO MLIYOPATA KWA MANUFAA YA TAIFA LA TANZANIA

09 Nov, 2022
Walimu wa michezo kutoka Shule Teule 56 za Michezo Tanzania wametakiwa kuyatumia vyema mafunzo waliyopata kuendeleza vipaji vya michezo katika shule wanazofundisha.
Rai hiyo imetolewa leo tarehe 9 Novemba, 2022 na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Leodegar Tenga alipokuwa anafunga mafunzo ya siku 7 kwa walimu hao yaliyoendeshwa na BMT uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.