KUREJEA KWA KIKOSI CHA TAIFA STARS

09 Sep, 2023
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere III, kutokea nchini Algeria baada ya mchezo wa kufuzu mashindano ya AFCON 2023, dhidi ya Algeria ambao ulimalizika kwa sare ya 0-0 na Stars kufanikiwa kufuzu baada ya kumaliza wapili katika kundi wakiwa na pointi 8 nyuma ya vinara Algeria wenye pointi 16.