MAFUNZO YANAENDELEA KWA SIKU YA PILI KWA MAAFISA UTAMADUNI NA MICHEZO

29 Aug, 2023
Maafisa Utamaduni na Michezo wakiendelea na Kikao kazi huku wakipata mada za kimkakati ikiwa ni siku ya pili leo Agosti 29, 2023 Mkoani Njombe.
Katika Kikao hicho maafisa hao wamepokea mada mbalimbali ikitanguliwa na mada ya Usajili wa vyama vya michezo kupitia mtandao iliyoanza kuwasilishwa Agosti 28 na kuhitimishwa leo Agosti 29, 2023 kutoka kwa wawasilishaji kutoka Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
Mada ya Nafasi ya Maafisa Utamaduni katika kukabiliana na Mmomonyoko wa MAADILI iliyowasilishwa na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Dkt. Juliet Kabyemera.
Huku mada kuhusu Mipango na Mikakati ya Maendeleo ya Michezo nchini, ikiwasilishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bw. Ally Mayay.