MAFUNZO YA RIADHA KWA WALIMU WA MICHEZO YAENDELEA ARUSHA

19 Jan, 2024
Afisa Maendeleo ya Michezo wa BMT na mtaalam wa mchezo wa riadha charles maguzu kwa niaba ya Baraza la Michezo la Taifa ameendesha mafunzo ya riadha kwa watoto (kids athletics) kwa walimu wa shule za Msingi na Sekondari za Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kupitia programu ya michezo kwa jamii (Sports Community) inayoratibiwa na BMT.
Mafunzo hayo yamefunguliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw. Seleman Msumi ambayo yataendeshwa kwa siku tatu kuanzia tarehe 18 hadi 20 Januari 2024 katika shule ya Turkish Maarifa iliyopo Jijini Arusha.
Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea utaalam walimu wapatao 132 walioshiriki ili waweze kuibua vipaji vya mchezo huo shuleni pamoja na kuongeza wataalam wa kusimamia mchezo huo nchini.