TIMU YA TAIFA YA MCHEZO WA KUOGELEA YATAKIWA KUHAKIKISHA INAPEPERUSHA VYEMA BENDERA YA TAIFA KATIKA MASHINDANO YA CANA ZONE 3 AFRIKA
service image
12 Nov, 2022

Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Tanzania Ally Mayay amewataka wachezaji wa Timu ya Taifa ya mchezo wa kuogelea kuhakikisha wanapeperusha vyema bendera ya Taifa katika mashindano ya CANA Zone 3 Afrika yanayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 16 Novemba, 2022 hapa nchini.

Mayay ametoa rai hiyo leo tarehe 12 Novemba, 2022 alipokuwa akikabidhi bendera ya Tanzania kwa timu hiyo,tukio lililofanyika katika moja ya kumbi za uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, ambapo pia amepongeza wazazi wa wachezaji wa kuogelea kujitoa kwa karibu kuendeleza vipaji vya watoto wao.

“haya ni mashindano makubwa sana kuwahi kufanyika kwetu hivyo niwasihi wachezaji hakikisheni mnalipambania taifa katika mashindano haya kuhakikisha kuwa mnapeperusha vyema bendera yetu ya Taifa na ushindi unabaki nyumbani,”amesema Mayay