MAFUNZO YA MFUMO WA USAJILI KIDIGITALI

28 Aug, 2023
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo (BMT) Bi. Neema Msitha leo Agosti 28, 2023 akitoa ufafanuzi wa umuhimu wa mafunzo ya mfumo wa usajili wa vyama vya michezo kidigitali (Sars) kabla ya mafunzo hayo kuanza ikiwa ni sehemu ya kikao kazi cha Maafisa michezo na Utamaduni kilichofunguliwa asubuhi na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Saidi Yakubu Mkoani Njombe.