MAFUNZO YA MFUMO WA USAJILI KWA VYAMA VYA MICHEZO KIDIGITALI (SARS)
service image
29 Aug, 2023

Maafisa Michezo na Maafisa Utamaduni ambao ndio waratibu na wasajili wasaidizi wa taasisi za michezo katika ngazi za Halmashauri leo Agosti 29, 2023 wameendelea kupata dozi ya mfumo wa usajili wa vyama vya michezo kidigitali (Sars) Mkoani Njombe.

Mafunzo ambayo yanayoratibiwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) yenye lengo la kurahisisha zoezi la usajili wa vyama vya michezo kwa kutumia mtandao popote alipo mteja badala ya kusafiri hadi zilipo Ofisi za BMT.

Mteja anayetaka kusajili chama cha michezo kwa sasa anaweza kujisajili kupitia Sars.bmt.go.tz au www.bmt.go.tz.