TUZO ZA BMT 2023

Bondia Yusufu Changalawe amefanikiwa kushinda tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka 2023 katika tuzo za baraza la michezo la taifa BMT zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Super Dome, Masaki.
Katika tuzo hizo ambazo mgeni rasmi alikuwa waziri mkuu wa Jamhuri muungano wa Tanzania, Majaliwa Kasim Majaliwa huku zikilenga kuongeza hamasa kwa wachezaji kujituma katika ushindani kupitia michezo wanayoishriki ndani na nje ya nchi.
Changalawe ameshinda tuzo ya mwanamichezo bora wa kiume kwa mwaka 2023 akiwashinda, Alphonce Simbu kutoka kwenye riadha na Pius Mpenda bondia kutoka katika ngumi za kulipwa.
Ushindi wa Changalawe umechagizwa na kufanya vizuri katika michuano ya Jumuiya ya Madola yaliofanyika Uingereza akirejea kwa kupata medali ya shaba.