TUZO ZA BMT 2023
service image
09 Jun, 2024

Bondia Grace Mwakamele ameshinda tuzo ya mwanamichezo bora wa kike wa mwaka 2023 akiwashinda Opa Clement kutoka mchezo wa soka na Madina Idd wa Gofu.
Mwakamele ameshinda kufuatia mwaka jana kushinda medali ya shaba katika mashindano ya Afrika nchini Cameroon.

Katika tuzo hizo ambazo mgeni rasmi alikuwa waziri mkuu wa Jamhuri muungano wa Tanzania, Majaliwa Kasim Majaliwa huku zikilenga kuongeza hamasa kwa wachezaji kujituma katika ushindani kupitia michezo wanayoishriki ndani na nje ya nchi.