TUZO ZITAENDELEA KUONGEZA HAMASA

Serikali imesema itaendelea kutoa tuzo, kwa wanamichezo ili kuleta hamasa na kuchochea ushindani wa ndani na nje ya mipika ya Tanzania.
Hayo yamesemwa leo Machi 17 na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Pindi Chana wakati wa kutoa tuzo kwa wanamichezo bora baada ya tuzo hizo kushindwa kutolewa kwa kipindi cha miaka 43 kwani tuzo za mwisho zilitolewa mwaka 1980.
Waziri wa Utamaduni, sanaa na Michezo anasema serikali itaendelea kutoa tuzo kwa wanamichezo waliofanya vyema kuhamasisha wanamichezo kufanya vyema na kuitangaza Tanzania kimataifa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la michezo la Taifa (BMT) leodegar Tenga amesema, tuzo za mwakani zitalenga pia kwa wachezaji wa zamani, ili kukumbuka mchago wao katika michezo nchini.