UONGOZI MPYA WA TWA

Chama cha wushu Tanzania (TWA) kimepata viongozi wapya ambao wataongoza katika kipindi cha miaka minne waliopatikana katika uchaguzi mkuu ambao umefanyika leo machi 23 ,2023 jijini Dar es salaam.
Viongozi hao ni pamoja na nafasi ya Mwenyekiti Mwarami Mitete aliyetetea nafasi yake mbaye amepata kura 32 dhidi ya mpinzani wake Ramadhani Ally Mshana aliyepata kura 24, Khalfan Mohammed Ally mgombea pekee ameshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa kura 49, huku nafasi ya Katibu Mkuu ikichukuliwa na Salehe Muhidini Mtaula ambaye ameshinda kwa kura 34 dhidi ya Mwinshehe koja mwenye kura 18.
Nafasi ya Katibu Mkuu Msaidizi imeenda kwa Azizi Ally Simba kwa kura 31 dhidi ya John Leo Lekule ambaye amepata kura 22, na nafasi ya Mweka hazina Hafidhi Abbasi Juma ameshinda kwa kura 30 dhidi ya Venance Mtamelo aliyepata kura 24.
Wengine ni Mweka hazina Msaidizi Omari Maisa amefanikiwa kushinda kwa kura 35 dhidi ya Stanford Jamal ambaye amepata kura 20, huku Mkurugenzi wa Habari imechukuliwa na Raphael Kallaghe ambaye ameshinda kwa kura 33 dhidi ya Mohammed Y.Mneka ambaye amepata kura 23.
Nafasi nyingine ni mkurugenzi wa mambo ya nje ambayo imeenda Sydool Mwigaya kwa kura 49, wakati Kawina Konde akishinda kwa kura 30 dhidi ya William D Ephrahim ambaye amepata kura 24 katika nafasi ya Mkurugenzi wa fedha, mipango na uwekezaji na Mkurugenzi wa Ufundi na Mafunzo imeenda kwa Juma Malenda ambaye amepata kura 35 dhidi ya Said Mfaume Salum ambaye amepata kura 19.
Wengine nafasi ya wajumbe ni Sophia S.Ngwaya, Abdalrahman Mtora, Afidhi Mandangwa, Hafidhi Kambangwa na Jeremia Martin.
Akizungumza mara baada ya uchaguzi huo Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Nicholus Mihayo amewataka viongozi hao kuhakikisha wanapitia mapungufu ya katiba yao na kuyafanyia maboresho, kuandaa mpango kazi na kalenda itakaonyesha matukio yatakayofanyika mwaka mzima, kuandaa semina, mkutano Mkuu, Mafunzo na mapambano ili kuendelea kikijenga chama.