VICKY ELIAS AING’ARISHA TANZANIA KATIKA MASHINDANO YA WAZI YA GOFU WANAWAKE 2023
service image
17 Sep, 2023

Mtanzania Vicky Elias amefanikiwa kuibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya wazi ya gofu wanawake 2023 yaliyofanyika katika viwanja vya Kiligolf Estate mkoani Arusha, baada ya kumshinda mtanzania mwingine Madina Iddi aliyeshika nafasi ya pili, Mercy Nyanchama akishika nafasi ya tatu na Ashley Awuor nafasi ya nne wote wakitokea nchini Kenya.

Mashindano hayo ambayo yamefanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 15 hadi 17 Septemba, 2023, yametumika kupata wachezaji watakaounda timu ya Taifa ambayo itashiriki katika mashindano ya Gofu Afrika Mashariki na Kati, yatakayofanyika mwezi Novemba, 2023 nchini Rwanda.