VIKAO VYA MAANDALIZI KUELEKEA MASHINDANO YA RIADHA YA WANAWAKE MSIMU WA NNE 2023
service image
06 Jan, 2023

Mtendaji Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha kwa kushirikiana Taasisi ya ushirikiano ya kimataifa ya Japan (JICA) wameendelea na vikao vya kimkakati kuelekea mafanikio ya mashindano ya riadha ya wanawake yanayotarajiwa kufanyika tarehe 21 hadi 22, Januari, 2022 Jijini Dar es salaam.

Mbio zitakazoshindaniwa katika mashindano hayo ni pamoja na Mita 100, 200, 400, 800, 1,500, 5,000, 10,000, 4*100 relay pamoja na kurusha mkuki (Javelin).

Kwa upande wa zawadi mshindi wa kwanza katika kila mbio ataondoka na kitika cha shilingi laki mbili (200,000), wa pili laki moja (100,000) na mshindi wa tatu ataondoka na shilingi elfu hamsini (50,000) pamoja na medali, huku mikoa mitatu itakayokuwa washindi wa jumla ikiondoka na makombe.