VIONGOZI WAPYA TTTA WATAKIWA KUWA WABUNIFU

Mwenyekiti wa uchaguzi wa Viongozi wa Chama cha Mpira wa Meza (TTTA) Charles maguzu amewataka viongozi waliochaguliwa leo Januari 07,2023 kwenye uchaguzi mkuu wa chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari kisutu kuwa wabunifu katika maeneo ya uongozi wa nafasi walizoomba kuziongoza.
"Kila mmoja aweze kuhakikisha kwenye kipengele chake cha uongozi kufanya mambo ya msingi ambayo yatasaidia mpira wa meza yanapiga hatua"
Waliochaguliwa katika uchaguzi huo ni pamoja na Mwenyekiti Buruani Mshale, Katibu Mkuu Agripina Habicht, Mweka hazina Michael Misabo, Yahya Mungilwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi na uendeshaji wa mashindano, Noorlain Sharrif Mwenyekiti Kamati ya watu wenye ulemavu na Anthony Mtafurwa Mwenyekiti Kamati ya Mipango, fedha na maendeleo.