VISIWANI WAJA KUPATA UZOEFU WA KUENDESHA MCHEZO WA NGUMI BARA
service image
03 Nov, 2022

Kamishna wa Idara ya Michezo Zanzibar, Ameir Mohamed Makame, akiambatana na Maafisa kutoka Baraza la Michezo Zanzibar (BMTZ) kwa ziara ya siku tatu kwa ajili ya kukutana na viongozi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) pamoja na Viongozi wanaosimamia mchezo wa ngumi nchini kutoka Kamisheni ya ngumi za kulipwa pamoja na Shirikisho la ngumi za Ridhaa ili kujifunza jinsi ya kuendesha mchezo huo visiwani  humo.

Akizungumza na waandishi wa habari Oktoba 03 Kamishna wa Idara ya Michezo Zanzibar,  Ameir Mohamed Makame, alisema kuwa lengo la kuja hapa Dar es salaam ni kwa ajili ya  kupata uzoefu kubadilishana mawazo na wenzao wa Bara hususani katika mchezo wa ngumi ili kuanza kwa mchezo huo Visiwani.

“Ikumbukwe Zanzibar imekuwa ikikataza kwa muda mrefu kujihusisha na mchezo wa ngumi lakini mwaka huu Baraza la wawakilishi limeruhusu sasa mchezo huu uanze kuchezwa rasmi hivi sasa tuko kwenye mchakato wa kuanza usajili wa vilabu na mashirikisho yake,”alisema Makame

“Tumeona ni vyema tuje huku kubadilishana mawazo na kupata uzoefu zaidi Siku hizi tatu tuweze kukutana nao wote ili tuone nini watatumbia kuhusu mchezo huu,” Alisema Makame.

Alisema pia wamekuja kuangalia changamoto wanazo kumbana nazo ili wajue jinsi ya kuzikabili lakini pia kuona miundombinu ya michezo hii.

Naye Afisa Maendeleo ya Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Milinde Mahona, alisema kuwa wamekuwa na kikao kizuri kama unavyojua Tanzania ina pande mbili Bara na Visiwani hivyo wanafanya kazi kwa kushirikiana katika sekta nyingi ikiwemo sekta ya michezo.

“Lilipokuja suala la ngumi wenzetu waliona waje watutembelee ili kuja kubadilishana uzoefu kama unavyojua sisi huku tumekuwa na utaratibu na mifumo tofauti ya kuboresha mchezo huu wa ngumi za wazi na ngumi za kulipwa waliona ni vema kabla ya kuanza wapate uzoefu,"alisema Milinde na kuongeza kuwa:

“Sisi tumewaambia mifumo
ilivyo na inavyofanya kazi tumewaeleza namna gani tunashirikiana na vyama hivyo ikiwemo utoaji wa vibali kwa matukio ya michezo kama ngumi hazifanyi kazi hadi zipate vibali kwenye kamisheni au shirikisho, muandaaji anapeleka ombi BMT.