WACHEZAJI WA JUMUIYA YA MADOLA WAPONGEZWA KWA KUFANYA VIZURI.

13 Aug, 2022
Timu ya Tanzania iliyoshiriki michezo ya 22 ya jumuiya ya madola na kufanikiwa kuleta medali tatu nyumbani yakaribishwa rasmi na waziri mwenye dhamana ya michezo Tanzania Mohamed Mchengerwa na kuwakabidhi vyeti wachezaji mashujaa walioshika nafasi kuanzia namba moja hadi nane kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola iliyomalizika hivi karibuni jijini Birmingham Uingereza.