WACHEZAJI WA KIKAPU WAENDELEA KUIPAMBANIA NCHI YAO
service image
20 Jun, 2023

Timu ya Taifa ya mpira wa kikapu (Tanzanites) inatarajiwa kutupa karata yake dhidi ya Rwanda katika mchezo wa tatu mashindano ya FIBA AfroCAN utakaochezwa tarehe 20Juni, 2023 majira ya saa moja usiku Kwenye Uwanja wa ndani wa Benjamini Mkapa.

Tanzania imeshacheza Michezo miwili ikiwa na ushindi wa vikapu 69 - 34 dhidi ya Eritrea huku tarehe 18 Juni, 2023 ilipoteza Kwa vikapu 77_63 dhidi ya Burundi.

Akizungumza mashindano hayo Kocha Mkuu wa Tanzania Mbwana Mohammed, alisema kuwa wamejipanga tayari kwa mchezo wa leo kuhakikisha wanapata Matokeo.

Àliwasihi watanzania wasivunjike moyo kwa matokeo ya kupoteza, bali wazidi kuiunga mkono timu yao, kwani vijana wanapambana kupata ushindi.

"Suala la maumbile kwa upande wetu ni madogo tukilinganisha na wapinzani wetu asilimia kubwa wanayo makubwa, lakini sisi tutapambana kwa uwezo wetu,"'alisema Mohammed.