WACHEZAJI WAKIKE MPIRA WA KIKAPU WAPIGWA MSASA
service image
16 Nov, 2022

Wasichana kutoka timu tofauti za mpira wa kikapu kutoka Dar es salaam wamepata mafunzo ya mchezo huo kutoka kwa balozi wa kimichezo kutoka nchini Marekani ambae pia ni mchezaji anayecheza ligi kuu ya mpira wa kikapu kwa wanawake nchini huyo (WNBA) Alysha Clark.

Mafunzo hayo yameendeshwa leo katika kiwanja cha mpira wa kikapu cha ocean road kwa uratibu wa
ubalozi wa marekani nchini Tanzania.

Naye makamu wa rais wa shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania, Lwehabura Munyagi ameeleza kufurahishwa na ugeni huo na kushirikiana nao kwa ajili ya mafunzo kwa watoto wa kike ambayo kutawapa fursa ya kucheza mpira wa kikapu pia kuwajengea mazingira mazuri ya kuweza kucheza mchezo huo.

"Jamii na wazazi waelewe kwamba watoto wa kike ni muhimu kushiriki mchezo huo sambamba na kujifunza ujuzi mbalimbali utakaowasaidia katika maisha yao lakini pia kupata udhamini wa elimu ya bure kupitia mchezo huo,"alisema Rwehabura.

Mafunzo hayo ni mwendelezo ambayo yalianzia Zanzibar, Dar es salaam na yatahitimishwa Jijini Arusha.