WALIMU WATAKIWA KUIBUA NA KUTENGENEZA VIPAJI VITAKAVYOKUJA KUSAIDIA TIMU YA TAIFA

05 Nov, 2022
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa (Mb), amesema msingi wa michezo nchini unategemea walimu wa michezo shuleni, kuibua na kutengeneza vipaji ambavyo vitakuja kusaidia timu mbalimbali za Taifa kufanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa.
Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo leo tarehe 5 Novemba, 2022 katika hafla ya ufunguzi wa mafunzo kwa walimu wa michezo kutoka shule teule 56 za michezo nchini yaliyoandaliwa na Baraza la michezo la Taifa (BMT),ambapo amewataka walimu kutumia vyema mafunzo wanayopata kwa manufaa ya maendeleo ya michezo nchini.