WANARIADHA WATAKIWA KUZINGATIA NIDHAMU MASHINDANO YA AFRIKA KWA VIJANA CHINI YA UMRI WA MIAKA 18 NA 20.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Y. Msitha, amewataka wanariadha wanaojiandaa na mashindano ya Riadha Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 18 na 20, kuzingatia nidhamu na Utamaduni wa kitanzania pindi watakapokuwa katika mashindano hayo.
Msitha ametoa rai hiyo leo Aprili 18, 2023 alipotembelea kambi ya timu ya Taifa ya Riadha inayojiandaa na mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kufanyika kuanzia Aprili 27 hadi Mei 3, 2023 nchini Zambia.
"Mtambue jicho la Serikali linatazama kwenu, hivyo tunatarajia makubwa, na sisi tunaendelea kufanyia Kazi mambo mbalimbali na kuyaweka sawa ili muende mkafanye vizuri katika mashindano haya makubwa Afrika," amesema Neema.
Timu hiyo inaundwa na wanariadha 15 wakike na kiume Kutoka Tanzania Bara na Zanzibar .