WASAJILI WASAIDIZI WAPEWA MAFUNZO YA USAJILI KUPITIA NJIA YA MFUMO WA MTANDAO
service image
11 Apr, 2023

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kupitia Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Michezo Tanzania, imeanza kutoa mafunzo ya usajili kwa kupitia njia ya Mfumo wa Mtandao, kwa wasajili wasaidizi ambao ni maafisa michezo wilaya nchini Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo tarehe 11 Aprili, 2023, katika ukumbi wa Arnautogluo uliopo Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, Msajili wa Vyama vya michezo Tanzania, Riziki J. Majala amesema mafunzo hayo yatafanyika kwa siku mbili katika Mkoa wa Dar es Salaam, ambapo lengo kuu ni kuwazesha maafisa michezo wilaya kufahamu namna ya kutumia mfumo mpya wa usajili utakaoanza kutumika rasmi mwezi Julai, 2023.