WASHINDI WA MANYARA TANZANITE MARATHON WATUNUKIWA

17 Dec, 2022
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT Bi. Neema Msitha akikabidhi zawadi kwa Washindi wa Mbio za Manyara Tanzanite Marathon KM 42, upande wa Wanawake zilizofanyika Disemba 17, 2022 Babati Manyara.
Mshindi wa kwanza katika mbio hizo ni Angelina Yumba kutoka Talent Arusha aliyekimbia kwa muda wa saa 2: 53:11, nafasi ya pili ni Tumu Andrea kutoka Singida aliyekimbia kwa muda wa saa 2:53:95 na watatu ni Vaileth Kudas kutoka Babati aliyekimbia kwa muda wa saa 2:56:55.
Washindi hao walikabidhiwa fedha taslimu pamoja na kuvalishwa Medali.