WASHIRIKI WA MAONESHO YA SABASABA KUTOKA WUSM WASHIRIKI MAZOEZI YA VIUNGO

11 Jul, 2023
Washiriki katika maonesho ya sabasaba ya 47 kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na taasisi zake tisa kwa kushirikiana na Wasafi media na klabu ya wasafi Jogging, julai 11, 2023 wameianza siku kwa mbio za barabarani kuendelea kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika michezo ili kuwa afya njema kwa ajili ya uchumi imara.