WATANZANIA WANG'ARA MASHINDANO YA MCHEZO WA VISHALE YA K.S.PRO AFRIKA.
service image
01 Aug, 2022

Wachezaji wa mchezo wa vishale Tanzania Subira Waziri na Anthony Florestine wamefanikiwa kuibuka washindi wa kwanza katika mashindano ya mchezo wa Vishale K.S PRO Afrika yaliyofanyika jijini Kampala nchini Uganda.



Kwa upande wa wanawake mchezaji Subira Waziri ameibuka kidedea baada ya kumfunga Balirwa Milly kutoka nchini Uganda katika mchezo wa fainali Tier 2 Series 3, wakati mchezaji Anthony Florestine yeye akiibuka mshindi wa Jumla kwa upande wa wanaume baada ya kumfunga Leto James wa Uganda katika mchezo wa fainali series 6.