YATENDEENI HAKI MAFUNZO MTAKAYOPATA
service image
27 Mar, 2023

Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha, amewataka wadau waliojitokeza katika mafunzo ya uamuzi na ukocha yaliyoandaliwa na Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA), kuyatendea haki mafunzo hayo watakaporejea katika vituo vyao vya kazi.

Rai hiyo ameitoa leo tarehe 27 Machi, 2023 alipokuwa anafungua mafunzo hayo uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, ambapo pia amepongeza Chaneta kwa kuendesha mafunzo kwani kunaonyesha ni jinsi Chama kipo hai, na wataalam watakaopata mafunzo watasaidia kuwaandaa wachezaji kuanzia ngazi za chini ili kuwa na timu nzuri ya Taifa itakayoleta ushindani katika mashindano ya kimataifa.

Mafunzo hayo yanashirikisha washiriki 70 kutoka katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania.