ZIARA
service image
22 May, 2024

Dkt. Serera afanya ziara ya kimkakati Misri.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Seleiman Hassan Serera leo Mei 22, 2024 amefanya ziara ya kimkakati katika kampuni ya ujenzi wa miundombinu ya michezo Cairo nchini Misri (The Arab Contractors) ili kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu michezo hasa katika suala la miundombinu.

Aidha, Dkt. Serera katika ziara hiyo amekutana na Meneja wa Kampuni hiyo pamoja na Meneja wa Kitengo cha Utawala na uhusiano Menna Yasser ambapo amefanya mazungumzo nao ya kina pamoja na kutembelea maeneo tofauti ya michezo yanayomilikiwa na Kampuni hiyo ukiwemo uwanja vya Mpira wa miguu, bwawa la kuogelea la kimataifa, na viwanja vya michezo tofauti ya ndani ambavyo hutumika kuwandaa wanamichezo akiwemo mchezaji maarufu wa Mpira wa Miguu Mo Salah.

Katika ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu aliambatana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya hamasa kwa timu za Taifa akiwemo Mwanahabari nguli Jemedari Said, Hamisi Ally na Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa BMT Bi. Najaha Bakari.

Dkt. Serera yuko Misri kama Mkuu wa Msafara wa Timu ya Taifa ya Mpira wa miguu ya watu wenye Ulemavu (Tembo Worriors) wanaoiwakilisha Tanzania katika michuano ya Afrika (AAFCON). Tembo Worriors inashuka dimbani kesho Mei 23, 2024 dhidi ya timu ya Ghana katika hatua ya robo fainali.