ZULFA APOTEZA HATUA YA 16 BORA DHIDI YA ADEIOLA KUTOKA NIGERIA
service image
10 Sep, 2023

Bondia Zulfa Macho amepoteza pambano lake la pili leo mchana dhidi ya bondia Adeiola Oyesiji kutoka Nigeria kwa points 5-0.

Zulfa aliyecheza vizuri round ya kwanza na kuongoza kwa points 3-2, alipoteza kwa points 5-0 katika round 2 za mwisho na hivyo kuitimisha safari yake ya kufuzu kwa Olimpiki ya Paris 2024 kwa Bara la Afrika.

Tanzania imebakiwa na wachezaji 4 ambao bado wanaendelea kusaka nafasi za kufuzu.

Baada ya Dakar, yatafuatia mashindano mawili ya kidunia ya kufuzu yatakayofanyika mwakani ambapo jumla ya nafasi 100 zitagombaniwa katika michezo itakayofanyika Busto Arsizio, Italy na Bangkok, Thailand.